MAKUNDI 10 YATINGA ROBO FAINALI YA DANCE 100% 2016 CHINI YA UDHAMINI WA VODACOM TANZANIA
Kundi la DDI Crew la jijini Dar es wakionyesha umahiri wao wakati wa shindano la robo fainali la Dance 100% 2016 lililofanyika katika viwanja vya Don bosco Oysterbay jijini,Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhanimiwa na Vodacom Tanzania.Jumla ya makaundi 10 kati ya 13 yalifanikiwa kuingia katika hatua ya nusu fainali itakayofanyika katika viwanja hivyo mwishoni mwa wiki.
Vijana wanaounda kundi la Mazabe Crew la jijini Dar es wakifanya mambo yao wakati wa shindano la robo fainali la Dance 100% 2016 lililofanyika katika viwanja vya Don bosco Oysterbay jijini, Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhanimiwa na Vodacom Tanzania.Jumla ya makaundi 10 kati ya 13 yalifanikiwa kuingia katika hatua ya nusu fainali itakayofanyika katika viwanja hivyo mwishoni mwa wiki.
Kikundi cha The Guest Crew la jijini Dar es Salaam, wakionyesha umahiri wao kusakata dance wakati wa shindano la robo fainali la Dance 100% 2016 lililofanyika katika viwanja vya Don bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam. Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhanimiwa na Vodacom Tanzania.Jumla ya makaundi 10 kati ya 13 yalifanikiwa kuingia katika hatua ya nusu fainali itakayofanyika katika viwanja hivyo mwishoni mwa wiki

TIMU MAKOROKORO: Kundi la timu Makorokoro Boys la jijini Dar es salaam, wakionyesha umahiri wao wa kusakata dance wakati wa shindano la robo fainali la Dance 100% 2016 lililofanyika katika viwanja vya Don bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam. Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhanimiwa na Vodacom Tanzania.Jumla ya makaundi 10 kati ya 13 yalifanikiwa kuingia katika hatua ya nusu fainali itakayofanyika katika viwanja hivyo mwishoni mwa wiki.

Kundi la J COmbaty la Zanzibar wakikonga nyoyo za mashabiki wakati wa robo fainali ya shindano la Dance100%2016 katika viwanja vya Don bosco jijini Dar es Salaam . Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhanimiwa na Vodacom Tanzania.Jumla ya makaundi 10 kati ya 13 yalifanikiwa kuingia katika hatua ya nusu fainali itakayofanyika katika viwanja hivyo mwishoni mwa wiki.

Kundi la Wazawa Crew la jijini Dar es Salaam,wakifanya manjonjo yao ya kudansi wakati robo fainali ya shindano la Dance100%2016 katika viwanja vya Don bosco jijini Dar es Salaam. Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhanimiwa na Vodacom Tanzania.Jumla ya makaundi 10 kati ya 13 yalifanikiwa kuingia katika hatua ya nusu fainali itakayofanyika katika viwanja hivyo mwishoni mwa wiki.

Kundi la Clever Boys la jijini Dar es Salaam, wakikonga nyoyo za mashabiki wakati robofainali ya shindano la Dance100%2016 katika viwanja vya Don bosco jijini Dar es Salaam . Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhanimiwa na Vodacom Tanzania.Jumla ya makaundi 10 kati ya 13 yalifanikiwa kuingia katika hatua ya nusu fainali itakayofanyika katika viwanja hivyo mwishoni mwa wiki.
TCW: Vijana wanaunda kundi la TCW Crews la jijini Dar es Salaam, wakikonga nyoyo za mashabiki wakati robofainali ya shindano la Dance100%2016 katika viwanja vya Don bosco jijini Dar es Salaam, Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhanimiwa na Vodacom Tanzania,Jumla ya makaundi 10 kati ya 13 yalifanikiwa kuingia katika hatua ya nusu fainali itakayofanyika katika viwanja hivyo mwishoni mwa wiki.
Mashabiki wa kudansi wakifuatilia mchuano mkali wa shindano la robo fainali ya Dance 100% 2016 katika viwanja vya Don bosco jijini Dar es Salaam,Uliokutanisha makundi 13 na kumenyana na makundi 10 kuingia hatua ya nusu fainali itakayofanyika katika viwanja vya Don bosco Oysterbay wiki ijayo chini ya Vodacom Tanzania na EATV.
Baadhi ya mashabiki wa kudansi wakifuatilia mchuano mkali wa shindano la robo fainali ya Dance 100% 2016 katika viwanja vya Don bosco jijini Dar es Salaam,Uliokutanisha makundi 13 na kumenyana na makundi 10 kuingia hatua ya nusu fainali itakayofanyika katika viwanja vya Don bosco Oysterbay wiki ijayo chini ya Vodacom Tanzania na EATV.
WARSHA YA KIMATAIFA KUHUSU MPANGO WA TAKWIMU ZA MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dk. Aziz Ponary Mlima akihutubia kwa niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi wakati akifungua warsha ya kimataifa kuhusu mpango wa takwimu za malengo ya maendeleo endelevu uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk.Alibina Chuwa (kushoto), akihutubia katika warsha hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shaban (katikati), akipitia nyaraka kwenye warsha hiyo. Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
Warsha ikiendelea.
Wadau wa maendeleo wakiwa kwenye mkutano huo.
Wadau wakifuatilia mada kwenye warsha hiyo.
Wanahabari wakiwa kwenye warsha hiyo.
Warsha ikiendelea.
Taswira ya meza kuu kwenye warsha hiyo. Kutoka kulia Dk. Verena Knippel, Mratibu wa Shirika la Global Partinership, Sanjeev Khagram, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk.Alubina Chuwa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dk. Aziz Ponary Mlima, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shaban, na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
SERIKALI MKOANI SIMIYU YAAZIMIA KUWACHUKULIA HATUA WATENDAJI WANAOTOA TAKWIMU ZA UONGO
Na Stella Kalinga, SIMIYU
Serikali Mkoani Simiyu imesema haiko tayari kuwavumilia na kuwaacha katika vyeo na majukumu waliyonayo watendaji wanaotoa takwimu zisizo za kweli.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa ufunguzi wa mafunzo elekezi yaliyotolewa kwa Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo, yaliyofanyika jana Mjini Bariadi, kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kiutendaji, kwa kuwa baadhi ya viongozi hao wametoka katika sekta binafsi ambazo zina mifumo tofauti ya kitendaji na mfumo wa Serikali.
“Tunawezaje kukaa na Mtendaji ambaye ukimwomba taarifa za upungufu wa madawati anadanganya, idadi ya wanafunzi anadanganya, walimu anadaganya tutamchukulia hatua tu. Lazima tupeleke ujumbe kwamba taarifa za uongo hazina nafasi tena katika Mkoa wa Simiyu. Namwagiza Katibu Tawala Mkoa, aanze kuchukua hatua stahiki dhidi ya watendaji wote waliotoa taarifa zisizo za kweli hususani katika takwimu za wanafunzi, walimu, madawati na vyumba vya madarasa”, alisema Mtaka.
Mtaka amesema azma ya Serikali Mkoani humo ni kuhakikisha Nafasi za watendaji wasio waadlifu zinajazwa na watumishi waadilifu, wenye sifa na elimu ya kutosha waliopo katika Halmashauri za Mkoa huo.
Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amewataka viongozi hao wa Wilaya kubaini watumishi wenye sifa na uwezo wa kutekeleza majukumu ya Serikali katika maeneo yao na wawape fursa watumie talanta zao kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Pamoja na kubaini watumishi wenye sifa, viongozi hao wameelekezwa kuwachukulia hatua watumishi wanaopenda kufanya kazi kwa mazoea, ikiwa ni pamoja na kuwapangia majukumu yanayoendana na uwezo wao wa kufanya kazi.
Katika kuboresha ukusanyaji wa mapato, Mtaka ametoa wito kwa viongozi hao kuibua vyanzo vipya vya mapato na kusimamia ukusanyaji wa Mapato hayo kwa kuzingatia maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ya kutowabugudhi wananchi wanyonge na akawataka Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanatenga asilimia 10 ya mapato yao ya ndani kwa ajili ya kuimarisha vikundi vya uzalishaji vya vijana na wanawake
Sanjari na hilo Mtaka amewataka Viongozi hao wa Wilaya kutambua fursa za maendeleo katika maeneo yao na kuzitekelezafursa hizo kwa manufaa ya Wananchi walio katika maeneo yao.
Akizungumza baada ya mafunzo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe, Tano Mwera alisema mafunzo hayo yamemsaidia kumpa mwanga na dira ya utendaji katika nafasi yake hasa katika utaratibu wa mawasiliano na mahusiano kati ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa kwa Mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za Nchi, Nafasi yake kama Kiongozi wa Serikali Wilayani pamoja na Sheria na Miongozo ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Mafunzo hayo ya siku moja kwa Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri ambayo yaliongozwa na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini. yaliendeshwa na Makatibu Tawala Wasaidizi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Mkoa huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni