Lmchina
socially, economically and others
Jumanne, 16 Agosti 2016
SERIKALI IPO TAYARI KUCHUKIWA NA WAVIVU
Baadhiya Bodaboda za washiriki zikiwa zimepaki bila
kufanya kazi ya kubeba abiria ambapo wamiliki walikuwa kwenye mafunzo
Na Mathias Canal, Singida
Serikali imeeleza kuwa ipo tayari kuchukiwa na wananchi wavivu wasiotaka
kujishughulisha na Ujasiriamali, Kilimo, Uvuvi, Ufugaji na Biashara ili kukuza
pato la kaya zao.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa kufunga mafunzo ya usalama
Barabarani kwa Waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda wa Wilaya ya Ikungi
yaliyohusisha Kata ya Issuna na na Kata ya Mkiwa na kufanyika JMC Hotel
Kijijini Issuna B.
Katika mafunzo hayo yaliyochukua siku sita yamewakutanisha pamoja waendesha
Bodaboda 84 ambao wamefundishwa Alama na sheria zote za usalama Barabarani,
Upatikanaji wa leseni, Faida za kulipa kodi na somo la ujasiriamali, Polisi
jamii, Ulinzi shirikishi na elimu juu ya maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU)
na Ukosefu wa Kinga Mwilini (UKIMWI).
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mirajji Jumanne Mtaturu akisisitiza juu ya umuhimu wa mafunzo ya usalama barabarani.
Akiwahutubia wananchi hao Mtaturu amemshukuru Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuanzisha
ajira ya pikipiki kwani kwa kiasi kikubwa imesaidia kupunguza uhalifu na
kuandaa ajira kwa vijana wengi nchini hivyo kuachana na kujihusisha na mambo
yasiyo na tija kwa jamii ikiwemo kushinda vijiweni.
Amesema kuwa mafunzo hayo yanayotolewa na shirika lisilo la kiserikali la
APEC yatasaidia kupunguza ajali za pikipiki zinazosababishwa na uzembe wa
baadhi ya waendesha pikipiki katika Wilaya zote za Mkoa wa Singida.
Dc
Mtaturu amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
kwa kushirikiana na Mkuu wa Polisi Wilaya kuhakikisha madereva Bodaboda waliokwepa
mafunzo ya awamu hii wanasajiliwa ili
wahudhurie mafunzo yatakayorudiwa kwa awamu ya pili kwa Wilaya nzima, hivyo kwa
wale ambao hawatapata mafunzo hawataruhusiwa kuendesha pikipiki zao ili
kuepusha ajali mpaka pale watakapopata mafunzo.

Dc Mtaturu (Kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa APEC Respicius Timanywa zawadi ya kuku iliyotolewa na wahitimu wa mafunzo hayo
“Dereva bila elimu ni sawa na bunduki bila risasi,
hivyo nakuagiza mkuu wa Polisi kutowakamata kwa kosa la kutokuwa na leseni
angalau kwa kipindi cha miezi miwili wakati wanafuatilia leseni zao” Alisema
Mtaturu
Akizungumzia kuhusu alama za barabarani Mtaturu
alisema kuwa tayari ameshamwagiza Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri kufanya
mawasiliano na wakala wa barabara katika maeneo yote ambapo alama za barabarani
hazipo.
Ili kuvunja makusudi makusudi ya kuvunja sheria Mkuu
huyo amemuagiza Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) amuelekeze mkuu wa Trafiki Wilaya
(DTO) ambapo alisema kuanzia leo kila dereva wa pikipiki anapaswa kutembea na
kivuli cha cheti na leseni.
Mkurugenzi wa Taasisi inayojihusisha na kupunguza umasikini na kutunza mazingira nchini Tanzania (APEC), Respicius Timanywa akiwashukuru washiriki wote wa mafunzo hayo
Akisoma risala iliyoandaliwa na wahitimu wa mafunzo
ya udereva wa pikipiki Kata ya Mkiwa na Issuna Yohana Chawenda amezitaja changamoto zinazowakabili waendesha
bodaboda hao kuwa ni pamoja na kukabwa na kuibiwa pikipiki zao, Upatikanaji wa
leseni, baadhi ya abiria kukataa kuvaa kofia ngumu, Baadhi ya waendesha
pikipiki kukataa kushiriki mafunzo ya usalama barabarani, Baadhi ya wananchi
kuharibu alama za barabarani na Baadhi ya maafisa wa usalama Barabarani
kusimamisha pikipiki sehemu isiyo rasmi jambo ambalo linachangia kuongezeka kwa
ajali za barabarani.
Mkurugenzi wa Taasisi inayojihusisha na kupunguza
umasikini na kutunza mazingira nchini Tanzania (APEC), Respicius Timanywa, amesema kuwa lengo la Taasisi hiyo kutoa mafunzo hayo ni kupunguza ajali na
kuwaandaa vijana kujihusisha na ujasiliamali wa uendeshaji wa Bodaboda huku
wakiwa katika hali ya usalama.
Timanywa amesema kuwa mafuzno hayo yataendelea
katika maeneo mengine ili kutoa fursa kwa watanzania wote wanaopenda kushiriki
kwa ajili ya kujifunza kwa manufaa ya leo na kesho.
Zaidi sana amesema kuwa mafunzo hayo pia yamelenga
kuwafanya vijana waweze kumiliki fursa kubwa na kutengeneza faida kubwa iliwaweze
kulipa ushuru na kodi za serikali.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mirajji Jumanne Mtaturu akisisitiza jambo wakati wa kufunga mafunzo ya waendesha pikipiki.
Dc Mtaturu akionyesha kuku aliyokabidhiwa kama zawadi baada ya kukubali kuwa mgeni rasmi wakati wa kufunga mafunzo hayo
Baadhi
ya washiriki wa mafunzo ya elimu ya usalama barabarani wakionyesha
alama za barabarani walizozichora wao wenyewe kwa ajili ya kuashiria
kuelewa mafunzo waliyopatiwa

Mbunge wa Jimbo mkuranga Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Njopeka mara baada ya kufanya ziara ya kuwashukuru wananchi hao baada ya kumchagua kuwa mbunge wa jimbo hilo ambapo pia mbali na kushukuru anatumia mikutano hiyo kuhamasisha maendeleo na kuwataka kufanya kazi kwa bidii leo mkoani Pwani.
Walimu wa shule ya msingi Misasa wakimsikiliza mbunge wa Jimbo la mkuranga Abdallah Ulega mara baada ya kuzuru shuleni hapo kwa lengo la kuwahamasisha kufanya kazi kwa bidii na kwamba yeye kama kiongozi wao yupo pamoja nao .
Akina mama wa kijiji cha Misasa kilichopo kata ya Likanga wakimsilikiliza mbunge wa Jimbo hilo Abdallah Ulega kwa makini wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru uliofanyika kijiji hapo ambapo pia walipata nafasi ya kuwasilisha changamoto zao hususani kukosekana kwa Zahanati na maji safi.
Watendaji wa halmashauri wakimsikiliza kwa makini mbunge wa jimbo hilo Abdallah Ulega,katika mkutano wake wa hadhara wa kushurukuru wananchi wa kijiji cha Njopeka ,kata ya Likanga ambapo katika ziara hizo amekuwa akitembea na watendaji hao ili kujibu hoja mbalimbali kutoka kwa wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akiwasili katika kijiji cha Misasa kilichopo kata ya Lukanga ,akiwa sambamba na baadhi ya viongozi wa kijiji waliokuja kumpokea,ulega yupo katika ziara ya kushukuru wananchi wake pamoja na kuhamasisha maendeleo ya watu.
Mbunge Abdallah Ulega akikabidhi madawati 537 kwa mkurugenzi wa halmashauri ya mkuranga Msham Munde ,madawati hayo yametokana na fedha zilizotolewa na bunge baada ya kubana matumizi na kukabidhiwa Rais Dkt John Magufuli ambaye naye aliagiza zitengeneze madawati.
Mdau wa maendeleo kutoka kampuni ya Hamisi Njomoke Limited akimkabidhi madawati 50 mbunge wa jimbo hilo Abdallah Ulega ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono kauli mbiu ya rais ya kuwataka watanzania kujitokeza kuchangia ili kuondoa kero hiyo katika shule leo mokani Pwani.
Mbunge Abdallah Ulega (katika alie simama) akiwa katika picha ya pamoja na mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya mkuranga Msham Munde, mkuu wa wilaya hiyo Filberto Sanga, na mdau wa maendeleo Hamisi Njomoke mara baada ya kukabidhi madawati 537 ya mbunge wilayani humo.
Sehemu ya madawati ya hayo. (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)
AWATAKA VIONGOZI NA WALIMU KUTUZA MADAWATI HAYO
Mbunge wa jimbo la mkuranga Abdallah Ulega amekabidhi madawati 537 kwa halmashauri ya wilaya hiyo, huku akiwataka viongozi wakiwamo madiwani wa kata mbalimbali kusimamia vizuri madawati hayo ili kutambua mchango mkubwa wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi alisema kuwa madawati hayo yametokana na fedha zao ambazo zilibaki baada ya kubana matumizi katika ofisi ya bunge na kwa kauli moja walikubali kumkabidhi Rais Dkt. Magufuli, ambapo naye kwa kutambua changamoto ya madawati akaelekeza fedha hizo zipelekwe kutengeneza madawati hayo.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Msham Munde alimshukuru Mbunge huyo na kudai kuwa uchangiaji wa madawati hayo ni mchakato endelevu hivyo wadau waendelee kujitokeza kuchangia huku akisisitiza kwamba kwa asilimia kubwa yamekwenda kutatua kero hiyo.
Wakati huohuo mdau wa maendeleo Hamisi Njomoke alimkabidhi mbunge wa jimbo hilo Ulega Madawati 50 kama sehemu ya kumuunga mkono mbunge paoja na Rais Dkt Magufuli huku akiwataka wadau wengine kujitokeza kuchangia ili watoto wasome katika mazingira rafiki.
by
lmchina.blogsport.com
ULEGA AKABIDHI MADAWATI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKURANGA.

Jumatatu, 15 Agosti 2016
MRS LUCY GOES TO AFRICA PREMIERS WITH A BANG IN DAR ES SALAAM
Wapenzi wa michezo ya kuigiza wakisubiri pazia lifunguke mchezo uanze
Mona Lisa katika taswira ya ufunguzi wa igizo hilo
Mona Lisa na "mumewe"
Nyumbani kwa Mona Lisa na mumewe
Kaka na dada wa nyumba ya Mona Lisa wakifanya yao jikoni
Mrs Lucy anawasili uwanja wa ndege na kushangaa kujikuta Afrika
Mrs Lucy anaanzisha rabsha uwanja wa ndege, mhudumu wa hapo anasogea kumpa msaada
Mrs Lucy haamini kuwa yupo Afrika
Juhudi za kumtuliza hazizai matunda mara moja
Natasha, mwenyeji wa Mrs Lucy anatokea
Mrs Lucy haachi vituko hata wakati wa kula
Sehemu ya umati
Mrs Lucy kapelekwa sokoni Kariakoo
Mrs Lucy na mtoto wa mwenyeji wake wakiwa sokoni
Ngoma za utamaduni zilirindima wakati wa kubadili mtazamo wa jukwaa
Natasha akipozwa na "mkwewe" wakati yu mahututi hospitali
Kaka anamtembelea Natasha
Mrs Lucy akimfariji mwenyeji wake Natasha ambaye ana muda nfupi wa kuishi kutokana na kuugua saratani
Sehemu ya tamati ya igizo ni mshangao kwa kila mtu
Waigizaji wa mchezo wanafunga pazia
Nyota wa igizo na Muigizaji/Mtunzi na Mkurugenzi mtendaji wa TDE Lady Toussaint Duchess Campbell (Lady T) akitoa shukurani zake kwa wote
Jumapili, 14 Agosti 2016
TANAPA,NGORONGORO NA IDARA YA WANYAMAPORI SASA MWENDO WA KIJESHI
Gwaride la wahitimu wa mafunzo ya kijeshi kwa askari na maafisa wa Hifadhi za Taifa likiingia katika viwanja vya mazoezi katika kambi ya mafunzo ya Mlele wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi akipokea salamu ya utii kutoka kwa askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (hawapo pichani) wakati wa ufungaji mafunzo kwa askari na maafisa hao yaliyofanyika katika kambi ya mafunzo ya Mlele mkoani Katavi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi akikagua gwaride wakati wa kufunga mafunzo kwa askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro yaliyofanyika katika kambi ya mafunzo ya Mlele mkoani Katavi 
Askari na Maafisa wa Hifadhi wakipita kwa heshima mbele ya mgeni rasmi kwa mwendo wa pole na haraka wakati wa ufungaji wa mafunzo ya kijeshi waliyopata katika kambi ya mafunzo ya Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu kutoka mfumo wa kiraia.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi(kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi wakipokea salamu za heshima kwa kupiga saluti wakati gwaride likipita mbele kwa heshima wakati wa ufungaji wa mafunzo kwa askari wa shirika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA) na Maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya taifa Ngorongoro.
Bendi ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ikipita mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa ufungaji wa mafunzo ya kijeshi kwa askari na maafisa wa Hifadhi ,Mafunzo yaliyofanyika katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.
Askari na Maafisa wa Hifadhi za Taifa wakionesha umahiri katika matumizi ya silaha wakati wakionesha kwa vitendo mafunzo ya kijeshi waliyopata katika kambi ya Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu. 
Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Witness Shoo (kushoto) pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi Mtango Mtahiko wakifuatilia maonesho ya matumizi ya silaha kutoka kwa wahitimu hao.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akisherehesha wakati wa ufungaji wa mafunzo ya kijeshi kwa askari na Maafisa wa Hifadhi waliyopata katika kambi ya Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu.
Askari na Maafisa wa Hifadhi wakionesha umahiri katika matumizi ya silaha wakati wakionesha kwa vitendo mafunzo ya kijeshi waliyopata katika kambi ya jeshi ya Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi pamoja na Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ,Freddy Manongi wakifuatilia maonesho hayo. 

Askari na Maafisa wa Hifadhi wakionesha umahiri katika matumizi ya silaha wakati wakionesha kwa vitendo mafunzo ya kijeshi waliyopata katika kambi ya Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi akitizama matundu ya risasi zilizolengwa na mmoja wa askari wa uhifadhi waliohitimu mafunzo ya kijeshi katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi.
Wakufunzi wa Mafunzo ya kijeshi kwa maofisa na askari wa Hifadhi za Taifa wakitambulishwa mbele ya mgeni rasmi,(hayupo pichani).
Mhifadhi kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Lilian Magoma akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wenzake wa mafunzo ya kijeshi yaliyofanyika katika kambi ya Mlele iliyopo mkoani Katavi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi akitunuku vyeti kwa askari na maafisa wa uhifadhi waliohitimu mafunzo ya kijeshi katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Getrude Lyatuu akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo. 
Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro,Freddy Manongi akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo. 
Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Alexander Songorwa akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)Allan Kijazi akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akimkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi kuzungumza na wahitimu wa mafunzo ya kijeshi kwa askari na maofisa wa Hifadhi za Taifa .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo kwa askari na maofisa wa Hifadhi za Taifa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi na viongozi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi na viongozi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa katika pichaya pamoja na wahitimu wa mafunzo ya kijeshi yaliyofanyika katika kambi ya Mlele mkoani Katavi. Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog ,Kanda ya Kaskazini.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)